Ni Vita Ya Europa League Ni Borussia Dortmund Na Liverpool Ya Jurgen Klopp Zijue Mbinu Za Timu Hizi.

Europa League.
Michuano ya Europa League inaendelea leo katika hatua ya Robo fainali katika viwanja vinne kuwaka moto macho na masikio ya wengi ni katika uwanja wa Signal Iduna Park wenyeji klabu ya Borrusia Dortmund watakuwa nyumbani kwa mara ya kwanza watamkaribisha kocha wao wa zamani Jurgen Klopp atakuwa na timu yake mpya timu ya Liverpool.
Uwanja wa Dortmund Signal Iduna Park Stadium.
Mchezo huu utachezeshwa na mwamzi wa kimataifa Carlos Velasco ndo atasimamia dimba la kati huku kila timu zikiwa na mfumo unaoendana kutokana na kocha wa sasa wa Dortmund Thomas Tuchel anaufahamu mfumo wa kocha wa zamani wa timu hiyo.

Refaree Carlos Velasco.
Kocha wa Dortmund anajivunia kwa kuwa na safu nzuri ya Ushambuliaji ikiongozwa na Raia wa Gabon Pierre na Reus na wakali wengine ambao hakika leo itakuwa mechi ya kusisimua kwa pande zote mbili kutokana na kuwa Dortmund wapo katika moto wa kuotea mbali hii ni baada ya kuitoa timu ya Uingereza ambayo na inaonekana kuwa bora timu ya Tottenham Spurs.
Kocha wa Dortmund Thomas Tuchel.
Kwa upande wa Jurgen Klopp atakuwa na kikosi ambacho kinaendelea kuuelewa mfumo wake na kina Countinho,Frimino na Lalana na wengine ambao watataka kuweka historia na hatimaye kuchukua kombe hilo ambako fainali itachezwa nchini Uswis.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp.
Mechi nyingine itakuwa katika uwanja wa Municipal De Braga nchini Ureno timu ya Sporting Braga watawakaribisha Shakhtar Donesk kutoka Ukraine.
Vita nyingine itakuwa katika uwanja wa El Madrigal manyambizi wa majano Villarreal watacheza Sparta Prague na katika uwanja wa San Mamea Barria timu ya Athletic Club wawaalika ndugu zao na mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Sevilla zote kutoka nchini Hispania.
Michezo hii itachezwa saa nne usiku kwa sasa za Africa Mashariki na tunatarajia kuona mechi nzuri na ngumu kwani hatua ya robo fainali na hatua ambayo haitabiriki kwa kila timu yoyote inaweza kushinda siku zote mpira wa mguu ni mchezo wa makosa.


  Published By: Alex Sonna.
 UnawezaKuzipata Story Zote Za Ndani Na Nje Ya Bongo Kwa Kujiunga Na SeetheAfricanLinkKwenye
:Facebook|Twitter|Instagram|YouTube|Audiomack
Powered by Blogger.