Ni Usiku Wa UEFA Champions League Ni Man City Na PSG,Je Real Madrid Kugeuza Kichapo Leo?Michuano ya Uefa ligi ya mabingwa barani Ulaya kuendelea tena leo kwa mechi mbili katika hatua ya Marudiano za Robo Fainali ya michuano hiyo. 
Baadhi ya wachezaji wa Man city.
Manchester City watakuwa wenyeji wa Paris St-Germain katika dimba lao la Etihad huku wakiwa wanatakiwa kushinda ama kuenda sare ambayo itawafanya waingie nusu fainali kwa mara ya kwanza,kwani mechi ya awali timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na kuwaweka pazuri kutokana na kuwa na faida ya mabao mawili.
Kikosi cha Psg.
Katika uwanja wa Santiago Bernabeu Real Madrid watakuwa na kibarua kigumu cha kugeuza kichapo cha 2-0 toka VfL Wolf-sburg walichokipata wiki iliyopita huku Wolfsburg wataingia kwa kujiamini huku Real wataingia kama nyuki kutokana na kufungwa mabao 2-0.
Kikosi cha Madrid.
Kikosi cha Wolfsburg.
Michuano hiyo itaendelea tena siku ya Jumatano Benfica watawakaribisha Bayern Munich ,na Atletico Madrid watakuwa wenyeji wa Barcelona.

 
Powered by Blogger.