Ni Marufuku Kutumia Tangazo La Mwanamitindo Aliyedhoofika Kiafya Lazuiwa.

Mwanamitindo aliyeathiriwa.
Kampuni ya Gucci imepigwa marufuku kutumia tangazo moja nchini Uingereza ambalo linamuonyesha modela mmoja aliyedhoofika kiafya.
Mamlaka ya viwango vya matangazo imeamua kwamba vile alivyosimama mwanamke huyo pamoja na alivyojipodoa kunamuweka aonekane kama aliyeathirika kutokana na ukosefu wa mlo.

Gucci iliitetea picha hiyo ikisema kuwa iliwalenga watu wazima na kusisitiza kuwa mwanamitindo huyo alikuwa mwembamba tu.
Lakini tangazo hilo haliwezi kutumika tena hadi litakapofanyiwa marekebisho.
Mamlaka hiyo imesema kuwa ilibaini kwamba kiwiliwili cha mwanamitindo huyo pamoja na mikono yake ilikuwa myembamba na haikuwa sawa na kichwa na eneo la chini la mwili wake.

''Pia tulibaini kwamba hisia za uso wake na vipodozi vyake vyeusi alivyopakwa hususan kandokando ya macho yake vinamfanya kuonekana aliyedhoofika.Kwa sababu hizo tumeamua kwamba mwanamitindo huyo aliyekuwa anategemea ukuta amedhoofika kiafya na kwamba tangazo hilo halina uwajibikaji''.

Wanaharakati wanasema kuwa mwanamitindo huyo wambemba kupitia kiasi wanaweza kuharibu kujiamini kwa wanawake na wasichana kupitia ukuzaji maumbile yalioathirika kiafya .
  Published By: Alex Sonna.

 Unaweza Kuzipata Story Zote Za Ndani Na Nje Ya Bongo Kwa Kujiunga Na SeetheAfricanLink Kwenye: Facebook|Twitter|Instagram|YouTube|Audiomack

Powered by Blogger.