Nani Kuingia Nusu Fainali Europa League Ni Vita Ya Liverpool Na Dortmund Hii Hapa Ratiba Yote.

Michuano ya Europa league kuendelea tena leo katika hatua ya mwisho wa robo fainali na kuingia katika nusu fainali viwanja vinne kuwaka moto.

Macho ya wengi wapenda kandanda Ulimwenguni kote ni katika uwanja wa Anfield kutakuwa na kazi kubwa pale wenyeji Liverpool watawakaribisha Borussia Dortmund huu mchezo utakuwa mgumu kutokana na mechi ya awali nchini Ujerumani timu hizi zilienda sare ya 1-1 na kuwafanya majogoo kuwa na faida ya bao la ugenini.
 Mechi nyingine zitakuwa Sevilla watacheza na na ndugu zao Athletic Bilbao mchezo wa kwanza sevilla walishinda bao 2-1 na kuwa na faida ya mabao mawili ya ugenini na kujiweka katika mazingira ya kutetea kombe hilo na kuweka rekodi ya kuchukua mara ya tatu na nchini Ukraine kutakuwa na mechi Shakhtar Donetsk watakuwa nyumbani kucheza na Braga Sporting na mechi ya awali Shakhtar kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuwa na faida ya bao mbili huku Sparta Prague watacheza na manyambizi wa majano timu ya Villarreal.


Powered by Blogger.