Mwanamuziki Chris Brown Asema Kuhusu Kujiua Kwake Kisa Nini Na Sababu Zake Zipo Hapa.

Chris Brown.
Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.
Katika kipande kifupi cha makala yake ya 'Karibu katika maisha yangu',mwanamuziki huyo wa mtindo wa R & B amesema kuwa uhusiano wao ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi kama hayawani.
''Nilikuwa katika kilele cha dunia,nyimbo zangu zikiongoza,nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa uma'',alisema.
Chris na Rihanna.

Brown alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kufuata shambulio hilo na kifungo hicho kilisitishwa mwaka jana baada ya jaji moja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake na kufunga kesi hiyo rasmi na kuwa huru.
Rihanna.
Makala hiyo inayowaonyesha Jennifer Lopez,Usher,Mike Tyson,Jamie Fox na Rita Ora,Chris Brown anasema kuwa ''Nilihisi kama nyota ,lakini nilijiharibia''.
''Nilikuwa nikilala.Sikuweza kula,nilijihisi maarufu'',alikisema Brown
Powered by Blogger.