Mkanda Wa Ngono Wampoza Karim Benzema Kutoshiriki Euro Mwaka Huu-FFF Yasema.

Karim Benzema.
Mshambulizi wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema, amepigwa marufuku ya kutoshiriki mashindano ya Euro2016 yanayotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.
FFF.

Shirikisho la soka la Ufaransa FFF limesema kuwa hakuna pingamizi kisheria linalomzuia mshambuliaji huyo asishiriki kindumbwendumbwe hicho ila kunahofu uwepo kwake katika timu ya taifa huenda ukahujumu mahusiano ya timu hiyo.
Aidha FFF linasema kuwa kuwepo kwake hakutatoa picha nzuri kwa mamilioni ya watu wanaomtazama.
Mchezaji wa Real Madrid

Benzema alipigwa marufuku mwezi Desemba mwaka uliopita baada ya kupatikana na hatia ya mkanda wa ngono.
  Mshambuliaji huyo anachunguzwa kwa madai kwamba alihusika katika njama ya kutishia na kudai pesa kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Ufaransa Mathieu Valbuena.
  Mathieu Valbuena.
  Kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps,ameiambia shirikisho la FFF kuwa anahofia Benzema ataidhuru motisha ya timu yake.
  Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps.

   


  Powered by Blogger.