Maumivu Azam FC Wachakazwa Na Waarabu Wa Tunisia Na Kutupwa Nje Ya Kombe La Shirikisho.

Azam fc.
Wakicheza katika uwanja wa Olimpic mabingwa wa Africa Mashariki na Kati na wawakilishi wa michuano ya kiombe la shirikisho timu ya Azam walishindwa kutamaba ugenini hii ni baada ya kukubali kufungwa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Esparence ya Tunisia mchezo ukichezwa usiku katika mji wa Tunis.
Farid akijaribu kuwatoka wachezaji wa Esparence.
Wakicheza kwa kujaza viungo Azam walihimili kipindi cha kwanza cha kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo uliokuwa mkali huku wenyeji wakilisakama lango la Azam kama nyuki pongezi ziende kwa mlinda mlango wao Aish Manula aliyefanya kazi kubwa ya kuzuia mabao kioindi hicho cha kwanza wenyeji walipata corne 8.
Kipindi kilianza kwa kasi huku wenyeji wakitafuta mabao la mapema ilikuwa dakika ya 48,64 na 81 wenyeji walipata mabao hayo kipindi cha pili na kuwatoa wana rambaramba hao na kwa matokeo hayo Azam imeyaanga washindano hayo kwa jumla ya mabao 4-2 kutokana mechi ya kwanza walishinda 2-1 Azam na kupelekea kutupwa nje ya michuano hii na Esparence wamefuzu kuingia hatua ya 16 ambapo wanasubili timu kutoka ligi ya mabingwa ambazo zitashindwa kufuzu hatua ya makundi.

Powered by Blogger.