Man United 21 Watwaa Ubingwa Wa Ligi Kuu Ya Uingereza Huku Wakiwa Na Mechi 2 Mkononi.
![]() |
Wachezaji wa Man United wenye miaka 21. |
Hilo ndilo taji la tatu kwa kikosi cha Warren Joyce ndani ya miaka minne.
Ushindi huo unawafanya United wafikishe pointi 45 katika msimamo wa Ligi Kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 England baada ya kucheza mechi 20, wakifuatiwa na Sunderland yenye pointi 43 za mechi 22.
Sunderland imemaliza mechi zake, wakati Man United ina viporo viwili dhidi ya Southampton na Chelsea.