Man City Yaweka Rekodi,Yaichapa PSG Na Cristiano Ronaldo Apiga Hat Trick, Huku Zikitinga Nusu Fainali.

Kocha wa Man City Pellergrin.
Timu ya soka ya Manchester city imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya Michuano ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kuwafunga Psg ya Ufaransa jumla ya bao 1-0.

Wakicheza katika dimba lao la Etihad Manchester city walifanikiwa kuandika bao pekee na la ushindi Dakika ya 76 kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji wao Kevin De Bruyne.
Kevin De Bruyne.
Kwa ushindi huo Manchester city wameifunga Psg jumla ya mabao 3-2 baada ya timu hizo kufungana bao 2-2 katika mchezo wa awali na kuweka rekodi ya mara ya kwanza kuingia nusu fainali tangu waanze kushiriki Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Katika uwanja wa Real Madrid imeichapa Wolf-Sburg 3-0 kupitia mabao ya mchezaji Christiano Rolnado ikiwa ni Hat trick yake katika mchezo huo.
Ronaldo.
Katika mchezo wa awali Wolf-Sburg walishinda 2-0 hivyo Real Madrid wamesonga mbele katika hatua ya Nusu fainali.
Michuano hii inaendelea tena leo kwa michezo miwili, Benfica itamenyana na Bayern Munich huku Atletico Madrid ikichuana na Barcelona katika dimba la Vicent.


 
Powered by Blogger.