Machafuko Yasababisha Ufaransa Kuvunja Uhusiano Wake Na Burundi.

Wakimbizi wa burundi.

Shirika la mataifa yanayozungumza lugha ya Ufaransa OIF limevunja ushirikiano wake na Burundi,likidai kushindwa kwa taifa hilo kupiga hatua ya mazungumzo ili kumaliza mgogoro unaoendelea.
Katika taarifa ,OIF limeshtumu hali mbaya ya usalama nchini humo na kusema kuwa linaondoa mipango yake yote isipokuwa ile inayowasaidia raia wa Burundi na zinaweza kusaidia kuimarisha demokrasia.Mataifa ya OIF ni 57 na serikali.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Zaidi ya watu 400 wamefariki huku takriban 250,000 wakilitoroka taifa hilo tangu ghasia kuzuka kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu.
Msemaji wa serikali ya Burundi amekuwa na hasira akijibu habari za kupigwa arufuku katika shirika hilo katika mtandao wa Twitter.Licha ya ushauri,alitumia lugha ya shirika hilo kulishtumu kwa kupuuza uwezo wake.
''Wanadhani wao ni mungu na Burundi ni lazima iliabudu shirika hilo.
Powered by Blogger.