Liverpool,Man united Na West Ham Zapeta,Tazama Msimamo Wa Ligi Hiyo Baada Ya Mechi Hizi.


ligi kuu England imeendelea kwa michezo mitatu kupigwa huku timu za West Ham, Liverpool,Man United wakishinda michezo yao.
 Wagonga nyundo wa West Ham wameibuka na ushindi wa maboa 3-1 dhidi ya Watford, mshambuliaji Andy Carrol, akifunga goli la kwanza dakika ya 11 kisha kiungo Mark Noble akifunga mabao mengine mawili kwa mikwaju ya penati.

Liverpool wakashinda deby yao kwa kuwachapa Everton kwa mabao 4-0, mabao ya majogoo hao yakifungwa na Divock Origi,Mamadou Sakho,Daniel Sturridge,Philippe Coutinho.

Nao mashetani wekundu wa Man United wakaibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace, beki Damien Delaney alianza kuipa Man United goli la kuongoza baada ya kujifunga kisha beki wa kiitaliano Matteo Darmian akaongeza bao la pili na kuipa timu yake alama tatu muhimu.

Kwa matokeo haya msimamo umekuwa hivi.

 
Nambari        Klabu Mechi          Mabao         Alama
1 Leicester 34 26 73
2 Tottenham 34 39 68
3 Man City 34 28 61
4 Arsenal 33 22 60
5 Man Utd 34 12 59
6 West Ham 34 14 56
7 Liverpool 33 13 54
8 Southampton 34 10 51
9 Stoke 34 -10 47
10 Chelsea 33 4 44
11 Everton 34 5 41
12 Watford 34 -7 41
13 Bournemouth 34 -16 41
14 West Brom 33 -9 40
15 Swansea 34 -11 40
16 Crystal Palace 35 -9 39
17 Norwich 34 -25 31
18 Sunderland 33 -18 30
19 Newcastle 34 -26 29
20 Aston Villa 34 -42 16
Powered by Blogger.