Liverpool Yaibamiza Vibaya Borussia Dortmund,Yatinga Nusu Fainali Ya Europa League,Matokeo Yapo.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp.

Ikicheza katika uwanja wake wa Anfield katika hatua ya Robo fainali ya michuano ya Europa imeendelea tena Alhamisi kwa michezo minne, ambapo Liverpool imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 4 -3 dhidi ya Borrussia Dortmund.
Magoli ya Liverpool yamefungwa na wachezaji Divock Origi, Philippe Coutinho, Mamadou Sakho na Dejan Lovren.
Na magoli ya Dortmund yamefungwa na Henrikh Mkhitaryan, Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus .
Sevilla imeiondoa Athletic Bilbao kwa changamoto ya penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 3-3 baada ya kila timu kushinda 2-1 mechi ya nyumbani.
Villarreal imeifunga Sparta Praga bao 4- 2 na Shakhtar Donetsk imeirarua Sporting Braga kwa mabao 4-0.
Kwa matokeo hayo Liverpool inaungana na Sevilla, Shakhtar Donetsk na Villarreal katika hatua ya nusu fainali.
 Powered by Blogger.