Liverpool Hoi Yabamizwa Na Villarreali Na Sevilla Yatafuta Rekodi Ya Europa League.

Countinho akiwa na wachezaji wa Villarreal.
Michuano ya Europa ligi iliendelea jana katika miji miwili tofauti katika hatua ya nusu fainali na fainali itachezwa mwezi wa tano mjini Basel nchini Uswis.
Wakicheza ugeninin vijana wa Jurgen Klopp wamechezea kichapo cha bao 1-0 toka kwa manyambizi wa majano Villarreal bao lao likipatikana kipindi cha pili dakika ya 70 likifungwa na Adrian.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Sevilla ikichezwa ugenini imetoka sare ya 2-2 na wenyeji Shakhtar Donetsk na kuipa nafsi timu ya Sevilla kusonga mbele na hatimaye kutinga fainali kutokana na kuwa na faida ya mabao mawili.
Powered by Blogger.