Leo Ni Kufa Kupona,Kisasi Cha FA Cup Simba Dhidi Ya Coast Union Katika Robo Fainali?

Hamis Kiiza na Beki wa Coast.
Michuano ya kombe la Azam Sport Federation hatua ya robo fainali kutafuta timu ya nne itakayoungana na Yanga,Azam na Mwadui kuendelea leo kwa mechi moja kuchezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Simba.
Timu ya Simba itakuwa nyumbani kuwakaribisha vibonde wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara klabu ya Coast Union kutoka jijini Tanga mchezo unaotabiriwa kutokuwa na upinzani kutokana na wagosi wa kaya kuwa katika kipindi kingumu kutokana na viongozi kuishusha morali timu hiyo kwa kuendekeza migogoro ambayo haina maana katika soka la Tanzania.
Kikosi cha Coast Union.
Timu yoyote itakayoshinda katika mchezo wa leo itaingia moja kwa moja katika hatua ya robo fainali ikiungana na Mwadui,Azam na Yanga na shirikisho la mpira wa miguu TFF litapanga ratiba ya nusu fainali ambapo mshindi wa kombe hili ataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Africa pamoja na kujinyakulia shilingi million 5,000,000.

SeetheAfricanLinkKwenye:
Powered by Blogger.