Kuelekea Mechi Ya Leo Azam Yapata Pigo Tunisia Na Yanga Vitani Kesho Dhidi Ya Waarabu Wa Misri.

Klabu ya Azam leo inaingia uwanjani majira ya saa 3;30 kwa Africa Mashariki katika michuano ya kombe la shirikisho huko Tunisia kucheza na wenyeji timu ya Esparance ukiwa ni mchezo wa marudiano mechi ya kwanza Azam walishinda kwa mabao 2-1 na kuelekea katika mechi wana rambaramba watawakosa wachezaji wake muhimu wa kutegemewa katika kikosi cha kwanza.
Tchetche Kipre.
Azam watamkosa mshambuliaji wao hatari raia wa Ivory Coast,Tchetche Kipre na mwenzake Pascal Wawa amabao wamekuwa na mafanikio katika kikosi hicho kukosekana kwa wachezaji hawa ni pigo kubwa kwa timu hiyo ingawa kuna wachezaji wengi wa kucheza katika nafasi zao kama Didier Kavumbagu na beki David Mwantika wanaweza  kuanza.
Pascal Wawa.
Mchezaji mwingine ambaye bado yupo katika majeruhi ambaye naye watamkosa huko Tunisia ni Shomari Kapombe ambaye mwaka huu ameonekana kuwa na mafanikio ingawa ni beki lakini kwenye msimamo wa wafugaji na yeye yumo akiwa na mabao 8,Timu ya Azam inahitaji ushindi kwa aina yoyote ili iweze kuingia 16 bora ama kutoka sare katika mchezo huu na uatakuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote mbili.
Shomari Kapombe.
Wawakilishi wengi katika michuano ya ligi ya mabingwa timu ya Yanga wao wajitupa uwanjani siku ya kesho majira ya saa 3;30 kwa Africa Mashariki hii ni mechi ya marudiano na mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Yanga.

Mchezo huu utakuwa mgumu kwa upande wa Yanga kutokana na kuwa Al-Ahly wana bao la ugenini na tangu klabu ya wana jangwani waanze kushiriki hawajawahi kupata matokeo mazuri mbele ya timu za kiarabu huku kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van Der Pluijm wametamba kuwa wataibuka na ushindi japokuwa historia haiwapi nafasi ya kusonga mbele ya michuano hii kutokana na kuwa na rekodi mbaya.
Kocha wa Yanga Hans Van Der Pluijm.
Kocha huyu amewataka wachezaji wake wacheze kufa na kupona ili waandike rekodi mpya katika maisha yao ya soka na pia ameeleza kuwa hatacheza kwa kujilinda bali watacheza kwa kushambulia na kukaba kwa pamoja na kuucheza mpira,Yanga wanahitaji ushindi au sare ya 2-2 ili waweze kutinga katika hatua ya makundi endapo watatolewa watakuwa na nafasi ya kucheza mtoano wa kombe la shirikisho.

Powered by Blogger.