Kuelekea Katika Mechi Ya West Ham Leo Ya FA Cup Louis Van Gaal Kayasema Haya.

Kocha wa Man United.
Klabu ya Man United leo itakuwa ugenini kucheza mchezo wa marudiano wa robo fainali ya FA watakuwa na kibarua kigumu mbele ya watoto wa London West Ham United na timu itakayoshinda moja kwa moja itaingia nusu fainali.

Louis Van Gaal.
Kuelekea katika mchezo huu kocha wa Man United Van Gaal ametamba kuwa leo wataibuka na ushindi kutokana na mechi ya awali kutoka sare ya 1-1 na kitu pekee cha leo ni kupata matokeo ambayo yatatufanya tufuzu hatua ya nusu fainali na hatimaye kuchukua ubingwa kutokana na kuwa katika wakati mgumu wa ligi kuu.
Kocha huyu ambaye anashtumiwa na mashabiki wa timu hiyo kuwa aondoke kutokana na United kutokuwa na matokeo mazuri katika ligi ya Uingereza na katika mechi ya leo wanaingia na kumbukumbu ya kufungwa 3-0 na Tottenham mechi ya Ligi.
Man United.
West Ham inaingia katika mchezo ikiwa imetoka sare ya 3-3 na Arsenal katika ligi na timu ya West wamekuwa wazuri mno wanapocheza katika uwanja wao wa nyumbani hivyo mchezo huu utakuwa mgumu kwani kwenye ligi hawajafungwa na timu kubwa mpaka sasa wakiwa katika uwanja huo.
Wachezaji wa West wakishangilia.
Powered by Blogger.