Viporo Vya Yanga Na Azam Na Kocha Wa Mwadui Julio Kihwelu Atamba Kuwafunga Yanga Taifa.

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kuendelea tena kesho kwa viporo viwili kuchezwa katika miji miwili nyasi zake kuwaka moto ni katika uwanja wa Taifa pamoja na Manugu Complex.
Yanga.
Katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kutakuwa mechi ya kukata na shoka timu ya Yanga watakuwa wenyeji wa timu ya kocha kwenye maneno mengi Jamhuri Kihwelo Julio timu ya Mwadui kwa mara ya kwanza wataingia katika uwanja wa Taifa.
Mwadui.
Mchezo huu unatabiriwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na mzunguko wa kwanza zilitoka sare ya 2-2 mjini Shinyanga na Mwadui wanaingia kwa kumbukumbu ya kufungwa mechi mbili za ligi hiyo wamefungwa na Mtibwa 2-1 na Ndanda 2-1 hivyo watataka kufuta machungu kwa kuwafunga Yanga huku Wanajanwani hao wao walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kagera na tayari Julio katamba kuwa atawafunga Yanga.
Mtibwa Sugar.
Huko katika uwanja wa Manugu Complex Turiani timu ya Mtibwa Sugar watacheza na wana ramba ramba timu ya Azam huu na utakuwa mchezo wa kufa na kupona kutokana uhalisia wa timu hizi mbili zinapokutana mzunguko wa kwanza Mtibwa alilala bao 1-0 katika uwanja wa Azam Complex.
Azam.
Timu zote zinaingia uwanjani zikiwa na matokeo ya kutoka sare katika michezo yao ya mwisho ya ligi kuu ya vodacom Azam wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walibanwa mbavu ya 2-2 na Ndanda huku Mtibwa Sugar wakishindwa kuwafunga wana jelajela na kulazimishwa 1-1dhidi ya Tanzania Prinsons.

Michezo yote ya kesho itakuwa na upinzani mkali kwa kila timu Azam wanaingia kwa kutafuta ushindi ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kutafuta ubingwa na Mtibwa nao wakitafuta nafasi za juu na klabu ya Yanga inaingia kwa kutaka kupata ushindi ili iendelee kumkimbiza mpinzani wake wa jadi vinara wa ligi hiyo Simba ambao wana pointi 57 wakiwa wamecheza michezo 24 na Yanga michezo 21 wana pointi 53 na Azam wamecheza mechi 22 wana pointi 52.
Powered by Blogger.