Imetimia Emmanuel Okwi Tayari Kurejea Tena Simba.

Emmanuel Okwi.
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda na klabu ya Sonderjyske ya Denmark Emmanueli Okwi yupo mbioni kurejea tena Msimbazi kwa Mara nyingine.
Okwi.
Mshambuliaji huyu alijizolea umaarufu na kuwa kipenzi cha mashabiki wa wekundu wa msimbazi kutokana na mchango mkubwa pindi alipokuwa anaichezea klabu hiyo hata hivyo bado ana mkataba na timu yake ya Denmarka.
Okwi akiwa Denmarka.

Chini kwa chini mabosi wa Simba kama watafanikiwa kumrejesha okwi hivyo kutapelekea kumuacha mshambuliaji wao hatari kwa sasa Hamisi Kiiza na nafasi yake kuchukuliwa na Okwi
Hamis Kiiza.
Kwa sasa klabu hiyo inatafuta nafasi ya kuchukua ubingwa msimu huu wa ligi kuu ya Tanzania bara na inapigania kwa hali na mali kushinda michezo yote iliyobaki ishinde huku ikiombea adui zake wafungwe.
Okwi akiwa anatambulishwa Denmarka.
Emmanueli Okwi aliuzwa kwa dau la dola 110,000 kwenda kwenye timu ya Sonderjyske ya Denmarka ambako ameshindwa kuonesha kiwango cha juu cha kuushawishi uongozi uendelee kuwa naye.
Powered by Blogger.