Huyu Hapa Mchezaji Wa Azam Atajiunga Na Malaga Au Las Palmas Kesho Nchini Hispania.

Farid Mussa.

WINGA chipukizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid Mussa, kesho Ijumaa anatarajia kuondoka nchini hapa Tunisia kuelekea Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Winga wa Azam fc.

Farid atakuwa huko kwa takribani mwezi mmoja na atafanya majaribio katika timu za Malaga na Las Palmas zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchini humu na atarejea jijini Dara es Salaam May 19 mwaka huu msimu wa ligi ukiwa umeisha.

Powered by Blogger.