Hivi Ndivyo Viporo Vya Azam Vilivyochacha Huku Coast Union Dhahiri Inashuka Daraja,Jana Wamefungwa Tena.

Baadhi ya Wachezaji wa Azam.

Ligi kuu ya Vodacom  Tanzania bara iliendelea tena jana kwa michezo miwili kuchezwa katika miji ya Dar es salaam na Songea
Azam Fc wakicheza katika uwanja wao wa Azam Complex, walishindwa kutamba mbele ya  Ndanda Fc kwa kukubali sare ya mabao 2-2.
Ramadhani Messi.

Didier Kavumbagu.
Mabao ya Azam yalifungwa na Ramadhani Singano na Didier Kavumbagu huku mabao ya Ndanda yakifungwa na Atupele Green kwa mkwaju wa penalti nae Hemed Msumi aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la pili.
Maji maji nao wakachomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, baada ya mchezo huo Coastal Union wanaendelea kuburuza mkia wakiwa na alama 19 wakiwa wamecheza michezo 26 na kwa mtazamo wa kawaida dhahiri Coast kashuka daraja na hatashiriki msimu ujao.


  Published By: Alex Sonna.
 UnawezaKuzipata Story Zote Za Ndani Na Nje Ya Bongo Kwa Kujiunga Na SeetheAfricanLinkKwenye:Facebook|Twitter|Instagram|YouTube|Audiomack
Powered by Blogger.