Hii Hapa Ratiba Ya Nusu Fainali Ya FA Cup,Yanga Wapewa Wabaya Wa Simba.

ASF CUP.


Ilikuwa ikisubiliwa kwa hamu ile Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imefanyika jana huku timu za Coastal Union na Mwadui FC zikipata nafasi ya kucheza nyumbani.
Ester Chaburuma.
Katika droo hiyo iliyochezeshwa na mchezaji mstaafu wa timu ya a taifa ya wanawake (Twiga Stars), Esther Chaburuma, imewashuhudia vigogo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, Azam FC na Young Africans wakipata nafasi ya kucheza michezo hiyo katika viwanja vya ugenini.
Mwadui.

Azam FC.
Mwadui FC watakua wenyeji wa Azam FC katika mchezo unaotarajiwa kucheza Aprili 24, 2016 mjini Shinyanga, huku wagosi wa Kaya Coastal Union wakicheza dhidi ya Young Africans katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga siku hiyo hiyo.
Coast Union.

Yanga.
Michezo yote hiyo itachezwa mwezi huu tarehe 24 na washindi wa  Nusu Fainali, watakutana fainali ya kombe hilo itakayofanyika mwezi Mei, ambapo Bingwa wake ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF).


 
Powered by Blogger.