Hii Hapa Ratiba Ya Ligi Kuu Ya Uingereza,Arsenal Kesho Na Je Leicester City Kutangazwa Mabingwa Mbele Ya Man United.


Kesho ni siku ya Jumamosi tarehe 30/04/2016 Ligi kuu ya soka ya England inaendelea tena hapo kesho kwa michezo sita nyasi zake kuwaka moto kwenye miji tofauti tofauti.
Katika uwanja wa Everton ni wenyeji wa Bournemouth, huku vijana wa Benitez walio katika hali mbaya ya kushuka daraja Newcastle United wanawaalika Crystal Palace.
Stoke city watacheza  dhidi ya Sunderlandvwanaojikwamua kushuka daraja na Watford watachuana na Aston Villa.
Baada ya kuwabana Tottenham timu ya West Brom wanawaalika West Ham United, na vijana wa Wenger wanaolilia nafasi ya nne timu ya Arsenal watakuwa wenyeji wa Norwich city.
 Leicester city bado ni vinara  yenye alama 76,Tottenham alama 69,Man city alama 64 sawa na Arsena yenye alama 64.
Katika kushuka daraja kuna timu ambazo zipo katika hali mbaya kutokana na kuwa na pointi finyu ambazo zinaweza kushuka daraja ama la tayari Aston Villa wameshashuka daraja msimu huu.
Siku ya Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa mechi tatu kuchezwa timu ya Swansea City watakuwa nyumbani kucheza na Liverpool,Vinara wa ligi hiyo timu ya Leicester City watakuwa ugenini kucheza na Man United katika uwanja wa Old Traford mchezo huu unatazamiwa na wengi kwani Leicester City endapo watashinda wataweza kutangazwa mabingwa wapya msimu wa mwaka 2016.
Mechi nyingine itakuwa katika uwanja wa St.Marry timu ya Southmpton watawalika matajiri wa kutupwa klabu ya Man City wanaotafuta nafasi za kushiriki ligi ya mabingwa mwakani watakuwa na kazi kutokana na wenyeji kuwa katika kiwango cha juu.

Powered by Blogger.