Hii Hapa Ratiba Ya Ligi Kuu Ya Uingereza Wikendi Hii.


Ligi kuu ya England inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo sita viwanja kuwaka moto huku kila timu ikitafuta pointi muhimu ya kushinda na kuendelea kutafuta nafasi za juu na nyingine zikikwepa kushuka daraja.
Mchezo wa mapema utakuwa kati ya  Norwich itaikaribisha Sunderland huku Everton wao watakuwa wenyeji wa Southampton.
Baada ya kufungwa na Tottenham klabu ya  Man Utd watakuwa wenyeji wa vibonde wa ligi hiyo timu ya  Aston Villa katika dimba la Old Traford , Newcastlle inayotafuta kujinasua kushuka daraja itamenyana na Swansea city.
Timu ya  West Brom watawaalika Watford na The Blue Chelsea watakuwa darajani Stamford dhidi ya Manchester City ambao wametinga hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa.
Wachezaji wa Leicester Mahrez,Shinji na Vardy.
Jumapili kutakuwa na michezo mitatu kuchezwa Vinara wa ligi Leicester city watakuwa nyumbani kucheza na West Hamhuku Bournemouth watawaalika Liverpool ambao nao wametinga nusu ya Europa league baada ya kuwatoa Dortmund na klabu ya Arsenal baada ya kutoka sare ya 3-3 na West Ham itamenyana na Crystal Palace katika uwanja wa Emirates.

 Powered by Blogger.