Haya Ndo Maamzi Ya Mario Balotelli Kayasema Haya Kuhusiana Na Liverpool.

Mario Balotelli.

Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli amesema hataki kurejea klabu yake ya Liverpool baada ya kipindi chake cha mkopo klabu ya AC Milan kumalizika mwisho wa msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na klabu hiyo yake ya zamani Agosti kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Anfield.
Balotelli amehangaika na amefunga mabao matatu pekee katika mechi 19 alizocheza hata hivyo alicheza vyema sana mechi mbili za karibuni zaidi.
Mario.
"Ninataka kusalia Milan kwa sababu sikuwa na raha Liverpool na sitaki kurudi huko,” amesema Balotelli.
Mchezaji huyo, ambaye aliwahi kuchezea Manchester City, alianza kwenye kikosi cha Milan kilichopata ushindi wa 1-0 ugenini Sampdoria Jumapili.
Alihifadhi nafasi yake licha ya kuchapwa nyumbani 2-1 na viongozi wa ligi Juventus mechi iliyotangulia.
Mario Balotelli.
"Nimecheza vyema mechi zilizopita mbili na kuna sita zilizosalia kwangu kujidhihirisha,” ameongeza.
Balotelli alifunga bao moja pekee Ligi ya Premia akichezea Liverpool baada ya kununuliwa £16m kutoka Milan Agosti 2014.
Powered by Blogger.