Hatimaye Boko Haramu 800 Wajisalimisha Kwa Jeshi Nigeria.

Kundi la Boko Haramu.
Wapiganaji 800 wa kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram wamejisalimisha kwa jeshi la Nigeria.
Hatua hiyo inafuatia mpango mahsusi wa 'Operation Safe Corridor' unaolenga kuwapokea wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi ambalo limesababisha vifo vya maelfu ya raia wa Nigeria.
Chini ya mpango huo wapiganaji wanaojisalimisha wanachukuliwa na kufunzwa upya njia mbadala ya kujitafutia riziki.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa wanaamini kuwa kuwasamehe wapiganaji wa Boko Haram watakaotubu makosa yao.
Kwa sasa wamewekwa kwenye makazi maalum ambapo wanaendelea kupata mafunzo ya msimamo wastani wa kidini.
Baadaye ya mafunzo  mbinu mpya za kujitafutia riziki kabla ya kupewa mtaji wa kuanza upya maisha yao.
Hata hivyo kuna hofu iwapo jamii itakuwa tayari kuwapokea wapiganaji waliotekeleza maasi dhidi yao.
Wahanga wa maasi yao ndio wanaotarajiwa kuwa na wakati mgumu zaidi kuwapokea ama hata kuwasamehe wapiganaji hao wa zamani.
Eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria ndilo lililoathirika sana na mashambulizi ya Boko Haram.
Zaidi ya watu 10,000 waliuawa huku takriban wakaazi milioni moja wakitoroka makwao tangu uasi huo uanze yapata miaka 7 iliyopita.

  Published By: Alex Sonna.
 Unaweza Kuzipata Story Zote Za Ndani Na Nje Ya Bongo Kwa Kujiunga Na SeetheAfricanLink Kwenye: Facebook|Twitter|Instagram|YouTube|Audiomack

Powered by Blogger.