Hatimaye Barcelona Yavuliwa Taji La Ligi Ya Mabingwa Kwa Aibu Na Bayern Munich Yabanwa Ugenini.

Wachezaji wa Barcelona wakiwa na huzuni.


Klabu ya soka ya Barcelona Jumatano ilivuliwa rasmi taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Atletico Madrid huku Mabao yote ya Altletico Madrid yakifungwa na Antoine Griez-mann na bao la pili likifungwa kwa mara nyingine na Antoine kwa njia ya penalti .
Atoine Griezmann akishangilia kwa style ya kubembeleza mtoto.
Griezmann akifunga bao kwa penati.

Kwa matokeo hayo Atletico Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3 -2 baada ya awali kufungwa 2-1 na Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou.

Katika mchezo mwingine Bayern Munich imefakiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitoa Benfica kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa jana .

Mabao ya Benfica yamefungwa na Raul Alonso Rodriguez na Anderson Souza Conceicao , na magoli ya Bayern Munich yakifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller .
Hivyo Atletico Madrid na Bayern Munich zinaungana na Real Madrid ya Hispania pamoja na Manchester City katika nusu fainali ambayo droo yake itapangwa siku ya Ijumaa.

 Powered by Blogger.