Google Kutoa Intaneti Ya Bure Kwenye Vituo Vya Treni

Google-public-Wi-Fi 
 Kufuatia mpango wake wa kuzifanya huduma zake kupatikana kirahisi na kwa watumiajo wengi zaidi nchini India Kampuni ya Google imeongeza mitambo mipya ya huduma ya intaneti bila waya (Wi-Fi) kwenye zaidi ya vituo tisa vya treni.
Google iliwasha mtambo wake wa kwanza mwezi Januari kwenye kituo cha Mumbai Central Station, ikishirikiana na shirika la Reli la India na kampuni ya RailTel. Huduma hiyo inayomuwezesha mtumiaji wa mtandao wa internet kutumia huduma hiyo bila kuunganisha waya wala kuwa na laini ya simu inatolewa bure kwenye vituo vifuatavyo:- Bhopal, Bhubaneshwar, Ernakulam Junction, Kacheguda, Pune, Raipur, Ranchi, Vijayawada naVishakhapatnam.
Baada ya kuviwezesha vituo hivyo kampuni ya Google imesema muendelezo wa kuongeza mitambo mingine itawezesha zaidi ya watu milioni moja na laki tano(1,500,000) kutumia huduma ya intaneti bila malipo kila siku.
Sababu kubwa ya kuweka huduma hii tena ikiwa bila malipo ni kutaka kurahisisha huduma ya usafiri wa treni nchini humo kwani abiria wanaweza kuangali ratiba za treni,kubadilishana maudhui kama vile kuangalia na kutumiana video wakati wa safari, Abiria pia wanaweza kutumia huduma hiyo kuagiza vyakula wakitumia Apps za migahawa ya vituo husika.
Powered by Blogger.