Dudu Baya Kuhusu Ujio Wake Mpya,Nyandu, Beef na Mr Nice Je?

Huyu hapa Dudu Baya mbele ya meza iliyopo #ubaoni je ni kweli amewaomba msamaha  wote aliowakosea? TUNE IN @efm_93.7  #huumchezohauhitajihasira
                 Dudu Baya amyasema hayo alipokua akipiga story na kipindi cha ubaoni ya 93.7Efm.

Mkongwe wa Muziki wa Bongoflava Dudu Baya "Mamba" amepiga stori na watangazaji Emma, Mpoki Na Bikira wa kisukuma (Seth).
 Alianza kwa kumuongelea mtoto wake  alipopigwa swali na Mpoki, 
 Mtoto wake ana Umri wa miaka (15) anaishi Dar Es Salaam Na Mama yake hajawahi kuishi nao lakini wanawasiliana mara kwa mara.
 Beef na Mr. Nice iliisha kitambo sasa ni muda wa kazi.
 Alipoulizwa kuhusu Nyandu Tozzy,
Dudubaya alisema alichokosea Nyandu Tozzy ni Kubadili Jina kutoka Dogo Hamidu kwani baadhi ya watu wanamuulizia (Waliomzoea kwa jina la Dogo Hamidu) hawalijui jina lake jipya.
  "Pamoja na yote najivunia kumlea amekua mkubwa na familia yake, ana mtoto sasa" 
 Dudu Baya ameongelea pia  Ngoma Yake Mpya "Kokoriko"
 Amesema huu ni ujio mpya wa Dudubaya ambapo Hivi sasa anashughulikia Video ya ngoma hiyo "Kokorikoo"
  mashabiki wake wanatakiwa wajiandae kwa vitamu.
 Kwani tayari ameandaa nyimbo tatu ziko tayari. 
 Hivi sasa Dudu Baya anafanya #DarEsSalaamTour  ambayo Wikiendi hii inaanzia Club Kakala Kigamboni.
Alipoulizwa nani Mkali kati ya Diamond na Ali Kiba Dudubaya alijibu swali hilo kiutu uzima kwa kusema wote ni wakali zaidi kwa  sababu kila mmoja anafanya muziki tofauti na mwenzake. Dudubaya alimalizakwa kusema hivyo.

Unaweza Kuisikiliza Na Kuipakua Hapa Ngoma yake Mpya (Kokoriko)
 

 
Powered by Blogger.