Kuelekea Mechi Ya Europa League Leo Kocha Wa Liverpool Jurgen Klopp Kayasema Haya.

Kocha wa Liverpool.
Michuano ya Europa League kuendelea leo katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo fainali yake itachezwa katika mji wa Basel nchini Uswis viwanja viwili kuwaka moto.
Liverpool.
Kikosi cha Liverpool tayari kimetua nchini Hispania kucheza na timu ngumu Villarreal katika dimba la El Madrigal huku kocha wa Majogoo hao Jurgen Klopp ametamba kuibuka na ushindi ili aweze kujiweka katika hatua nzuri ya kutinga fainali na pia ametoa tahadhari kwa wachezaji wake wacheze kwa nidhamu kutokana na kuwa timu ya Villarreal ni wazuri sana wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Villarreal.
Mabingwa mara mbili wa kombe hilo na ndo mabingwa watetezi timu ya Sevilla watakuwa katika dimba la Arena Lviv nchini Ukraine kucheza na wenyeji timu ya Shakhtar Donetsk.
Sevilla.
Mchezo huu unatazamiwa kuwa mgumu kwa kila pande kutokana na wenyeji kutokuwa na matokeo mazuri mbele ya Sevilla huku vijana toka Hispania wakisaka nafasi nyingine ya kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.
Shakhtar Donetsk.

Powered by Blogger.