Barcelona Yachapwa Vibaya Na Valencia Katika La Liga Na Kubanana Koo Na Atletico Madrid Kileleni.

Wachezaji wa Barcelona.
Wakicheza katika uwanja wao wa Nou Camp timu ya Barcelona iliendelea kupata jinamizi la kugawa pointi baada ya kuchapwa na Valencia mabao 2-1 huu ni mchezo wa nne kupoteza baada ya kufungwa na mahasimu wa wakubwa Real Madrid 2-1,Real Sociedad 1-0 na pia ilipata kichapo katika ligi ya mabingwa cha mabao 2-0 toka kwa Atletico Madrid.
Ivan Rakitic.
Valencia walipata bao la kuongoza mnomo dakika ya 26 baada ya kiungo mshambuliaji wa Barcelona Ivan Rakitic kujifunga baada ya kuona hivyo timu ya Barelona waliendelea kulishambulia lango la Valencia huku wakichezaji kwa kasi mshambuliaji wa wageni Santi Mina alieandika bao la pili na la ushindi kunako dakika ya 45 kipindi cha kwanza hadi mapumziko Valencia 2-0.
Santi Mina.
Kipindi cha pili kilianza huku barcelona wakitafuta kurudisha mabao hayo waliendelea kushambuliana kwa kasi mnamo dakika ya 60 Lionel Messi aliipatia bao la kufutia machozi timu yake hadi dakika 90 Valencia wameibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Lionel Messi.
Kwa matokeo haya Barcelona wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na pointi 76 wakilingana na Atletico Madrid wenye pointi 76 wakiwa na tofauti ya kufungwa na kufunga huku nafasi ya tatu Real Madrid wana pointi 75 na matokeo mengine Atletico Madrid wameibuka na ushindi wa 3-0 na Real Madrid wakishinda mabao 5-0.

Powered by Blogger.