Baada Ya Kununua Nyumba Africa Kusini,Msanii Diamond Platnumz Kayasema Haya Kuhusu Marekani?

Diamond Platnumz.
Msanii Diamond Platnumz amefunguka kuhusu suala la yeye kutonunua nyumba nchini Marekani kama wasanii wenzake wakubwa wa Afrika wanavyofanya.

Diamond amefunguka hilo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa haoni umuhimu wa yeye kununua nyumba Marekani, tofauti na alivyonunua Afrika Kusini, kwani kule ilimlazimu.

Diamond akiwa na mke wake Zari.


“Nina nyumba South Africa kwa sababu nina familia South Africa kwa hiyo ni lazima ninunue nyumba south Africa, lakini sina sababu ya kusema ninunue nyumba Marekani, ninunue nyumba Marekani kwa sababu gani, kwanza sipapendi, uongozi unajua kabisa”, alisema Diamond. Pia Diamond aliweka wazi kuwa kununua nyumba Marekani kwake hakuna faida, ni heri awe na kijiji cha nyumba Tandale au Mwananyamala, lakini si Marekani.

Diamond na Zari.


“Nyumba sio hela nyingi dola laki mbili kama milioni mia nne unanunua nyumba, so ni matakwa ya mtu mwenyewe, sasa usitake kununua nyumba Marekani wakati trip zako za kwenda Marekani ni chache, usitake kuonekana tu una mashauzi, mara kumi milioni 500 ukanunua nyumba pale Tandale karibuni 10 ukapost nna kijiji Tandale ukazipangisha ukaingiza hela kuliko Marekani”, alisema Diamond.


Dangote A.K.A Simba.
Powered by Blogger.