Baada Ya Kufutwa Kazi Jose Mourinho Pale Chelsea Yameibuka Mapya,Cesc Fabregas Kayasema Haya.

Jose Mourinho.
Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas amesema Jose Mourinho alikosa kufanikiwa Stamford Bridge msimu huu kwa sababu aliwaamini wachezaji kupita kiasi.
Mourinho, 53, alifutwa mwezi Desemba klabu hiyo ikiwa alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja.
Jambo la kushangaza ni kwamba miezi mmoja awali, Mourinho alikuwa amewaongoza kushinda taji la Ligi ya Premia.
Fabregas, 28, sasa anasema wachezaji walikosa kufanya hisani baada ya kuongezewa muda wa kukaa likizoni kama zawadi kwa kushinda ligi.
“Namheshimu sana Mourinho,” Fabregas aliambia Sky Sports.
Cesc Fabregas.
"Tatizo kubwa ni kwamba alikuwa na imani sana nasi, aliongezea likizo kwa sababu tulikuwa tumeshinda ubingwa lakini hatukumtendea hisani, tulimsaliti.
Fabregas.
"Hiyo ndiyo sababu kuu akafutwa, na kwa sababu ya hilo mimi na wachezaji wengine katika timu tunajilaumu.”
Powered by Blogger.