AZAM YATOA FURSA KWA WENYE VIPAJI KUPITIA MRADI WA "KIWANDA CHA FILAMU"
Azam Tv kupitia chaneli yake ya Sinema Zetu leo Jumanne
19/4/2016 imezindua rasmi mradi wake unaojulikana kama “Kiwanda Cha Filamu”.msamimzalishaji
Akiongea mbele ya waandishi wa habari meneja mauzo na masoko
wa Azam Bw. Kiwanga Mgope amesema lengo la kuu la mradi huu ni kukuza na kuinua
vipaji vya wasanii toka nchini ambao bado hawajapata fursa yakuonyesha kazi zao
katika jamii. Washiriki wa mchakato huu ni kuanzia umri wa miaka 18 na
kuendelea.
Naye mzalishaji na msimamizi wa mradi huu Zamaradi Nzowa
amesema Usahili utakuwa ni wa siku nne, Usahili wa kwanza ni siku ya Jumatano
wiki hii ya tarehe 20 Aprili pale Coco Beach kuanzia saa 3 asubuhi, usahili huo
utawashirikisha washiriki zaidi ya 200 ambao tayari wanajua kuwa kesho
watakutana, Washiriki watapimwa viwango vya vipaji vyao kupitia script ya kazi
ambayo imekwishaandaliwa.
Majaji katika usahili huo atakuwa msanii maarufu na mkongwe
katika tasnia ya uigizaji Bi. Susan Lewis almaarufu Natasha akiwa na Bw. Issa
Mbura msanii muigizaji aliyejipatia umaarufu katika filamu ya “Home Coming”
ambae pia ni Muhadhiri msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika sekta ya
luninga na filamu na kuwa mwalimu wa uigizaji na utayarishaji wa filamu. Katika
siku za usahili atakuwepo jaji mmoja mualikwa hivyo kufanya idadi ya majaji
kuwa watatu.
Washiriki ambao watashiriki kupata nafasi ya uigizaji na cameraman
wamepatikana baada kutakiwa kutuma kazi zao kwa whatsapp namba iliyokuwa
imetolewa, washiriki hawa ni kutoka nchi nzima.
Kiwanda cha Filamu kinatarajia kupata washindi 20 waigizaji
na wapiga picha za video 2, washindi hawa watapata fursa ya kuonekana katika
tamthilia mahiri na itakayo washirikisha wasanii maarufu katika sekta ya
uigizaji Tanzania chini ya chaneli ya Sinema Zetu. Tamthilia hii inatarajiwa
kuanza kutengenezwa rasmi mnamo mwezi Mei mwaka huu na kuzinduliwa mwezi Julai
mwaka huu, filamu hiyo itaitwa TAXI ambapo dereva wa Tax hiyo wananchi watapewa
nafasi ya kukisia dereva ni nani, na inasemekana kwamba ni mtu maarufu..
Washindi hao 20 waigizaji na cameraman 2 watapata fursa
yakupata elimu zaidi juu ya vipaji vyao kabla yakuanza kushiriki kwenye
tamthilia hiyo.
Pia wakati wa kufanyika filamu hiyo kutakuwa kukirekodiwa matukio yote yanayokuwa yakiendelea wakati kurekodo yani behind the scene ikifahamika kama "Kiwanda Kiwandani"