Angalia Mdhahalo Wa Hillary Clinton Na Bernie Sanders Walivyojibizana New York.

Sanders na Clinton.

Wagombea urais waliosalia katika chama cha Democratic, Hillary Clinton na Bernie Sanders, wamejibizana vikali katika mdahalo uliofanyika katika jiji la New York.
Kila mmoja ametilia shaka uwezo wa mpinzani wake kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala kama vile kudhibiti benki Wall Street, kudhibiti umiliki wa silaha na ujira wa chin huku jimbo la New York litafanya mchunjo wake siku ya jumanne.
Bw Sanders amemkosoa Bi Clinton kwa kuunga mkono vita vya Iraq na kutetea mikataba ya biashara huru
 Naye Bi Clinton amemtuhumu Bw Sanders na kusema hawezi kutekeleza hata sera zake mwenyewe, mfano kuvunja udhibiti wa benki kuu za Wall Street.
Bernie Sanders.


Wote wawili wana uhusiano mkubwa na jimbo hilo la New York Bw Sanders alizaliwa hapo huku Bi.Clinton amekuwa seneta wa jimbo hilo kwa miaka minne na mdhahalo huo wa runingani umefanyika eneo la Brooklyn.
Bw Sanders ameshinda majimbo saba kati ya manane yaliyofanya mchujo karibuni jambo lililomuwezesha kupunguza uongozi wa Bi Clinton katika mchujo wa chama hicho.
Hillary Clinton.
Bi Clinton hata hivyo bado anajivunia uongozi mkubwa huku uchaguzi mkuu wa Marekani utafanyika mwezi wa Novemba.

Powered by Blogger.