Angalia Ilivyotokea Wafanyakazi Hewa Wamponza Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga.

Bi.Anne Kilango Malecela.
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa.
Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.
Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya Uchuguzi huo bado unaendelea.
Rais John Pombe Magufuli.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa kazini mara moja.
Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani.
 

Powered by Blogger.