MPOTO AMLILIA SEMZABA


Msanii na mtunzi wa mashairi ya nyimbo za asili Mrisho Mpoto(Mjomba) leo ameshindwa kuvumilia baada ya kuangalia kilio wakati wa Ibaada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa vitabu Profesa Edwin Semzaba.
 Ibaada hiyo ilifanyika katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
 Huku akionyesha huzuni kubwa Mpoto amesema pengo la Semzaba ni kubwa sana kwenye tasnia ya uandishi.


"Semzaba kwangu ni zaidi ya mzazi kwani japokuwa sijasoma sana lakini nimeishi chuo kikuu kwa miaka zaidi ya kumi nikijifunza sanaa.Hivyo hata mafanikio niliyonayo ni kupitia yeye"
Alisema Mpoto.
 Marehemu Semzaba atakumbukwa kwa umahiri wake katika uandishi wa vitabu kwani hakuna Mwanafunzi ambae amefika sekondari halafu hakusoma hata kitabu kimoja cha Marehemu.

Picha Na: Omary Mgazza


Powered by Blogger.